Jeremiah 31:6-7


6 aItakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelele
juu ya vilima vya Efraimu wakisema,
‘Njooni, twendeni juu Sayuni,
kwake Bwana Mwenyezi Mungu wetu.’ ”

7 bHili ndilo asemalo Bwana: “Mwimbieni Yakobo kwa furaha,
mpigieni kelele aliye mkuu wa mataifa.
Zifanyeni sifa zenu zisikike, nanyi mseme,
‘Ee Bwana, okoa watu wako,
mabaki ya Israeli.’
Copyright information for SwhKC